BAADA ya kupoteza matumaini ya kumaliza ukame wa kutwaa vikombe kwa muda wa miaka sita iliyopita kufuatia kisago cha mabao 2-1 kilichotolewa huko Reebok Stadium, Kocha Mkuu wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amesema anastahili kualaumi yeye binafsi na si wachezaji wake.
Wenger alisema kijumla wachezaji wake wamejituma kikamilfu kwa muda wa msimu mzima hivyo hakuna haja ya kulaumiwa zaidi yake yeye ambae ndie mwenye jukumu la kuhakikisha ukame wa vikombe unamalizwa huko Emitrates.
Alisema kila shabiki anaeipenda Arsenal ulimwenguni atakua amechukizwa na matokeo yaliyopatikana jana hali amabyo inapelekea kuwalaumu wachezaji lakini bado ameendelea kusisitiza kuwa lawama za kushindwa kufikia melengo waliyojiwekea zinastahili kutupwa kwake.
Hata hivyo mzee huyo ameendelea kuwa na msimamo wake wa kutobadilisha mfumo wa kuwatumia vijana huku akidai kwamba bado anaamini mfumo huo ni mzuri na ipo siku utaleta mafanikio chini ya utawala wake.
Alisema ni vigumu kufanya maamuzi ya kubadilisha mfumo kutokana na matakwa ya mashabiki na kama atashawishiwa na yoyote yule anaeupinga mfumo wake kwa vielelezo sahihi atakua tayari kuubadili.
Kauli hiyo ya Arsene Wenger imepingwa vikali na beki wa zamani wa klabu ya Arsenal, Lee Michael Dixon ambapo amesema iwe isiwe ni lazima meneja huyo wa kifaransa akubalia kubadilika na kinyume na hapo ataendelea kuambulia patupu kila unapofika mwisho wa msimu.
Lee Michael Dixon amesema mfumo wa kuwategemea vijana unaotumiwa klabuni hapo tayari umeshajidhihirisha wazi hauwezi kuipa mafanikio Arsenal hivyo hakuna haja ya kuendelea kutumiwa zaidi ya kufanya usajili wa wachezaji waliokomaa.
Alisema ujio wa muwekezaji ndani ya klabu ya Arsenal unatakiwa kuchukuliwa kama faraja ya kumfanya Arsene Wenger kuiweka kando sera yake ya vijana.
Wakati huo huo Lee Michael Dixon ameikubali kauli iliyotolewa na nahodha wa klabu ya Arsenal Cesc Fabregas siku moja kabla ya mchezo wa ligi dhidi ya Spurs ambayo ilikaririwa na vyombo vya habari vya nchini kwao Hispania ikieleza kwamba ni wakati wa Arsenal kufanya maamuzi ya kutwaa vikombe ama kuendeleza makinda kama ilivyo sasa.
Lee Michael Dixon amesema kauli hiyo ina uzito wa aina yake na inajidhihirisha wazi kwamba ni vipi nahodha huyo alivyochoshwa na mwenendo uliopo klabuni hapo lakini pia akaeleza kwamba Fabregas hakustahili kulisema hilo hadharani kufuatia nafasi aliyonayo ndani ya kikosi.
Kufungwa katika mchezo wa jana mabao mawili kwa moja na Bolton Wanderers, kunadhihirisha wazi kwamba Man Utd wapo mbele kwa tofauti ya point 9 dhidi Arsenal ambao kwa sasa wanakamata nafasi ya tatu huku nafasi ya pili ikishikiliwa na Chelsea.
No comments:
Post a Comment