Saturday, April 23, 2011

NEUER KUIKIMBIA SCHALKE 04 MWISHONI MWA MSIMU.

MUNICH, Ujerumani
MLINDA mlango wa kimataifa toka nchini Ujerumani pamoja na klabu ya Schalke 04 Manuel Neuer ameonyesha nia ya kutaka kuihama klabu hiyo baada ya kugoma kusaini mkataba mpya pindi alipotakiwa kufanya hivyo.

Manuel Neuer amekataa kufanya hivyo huku ikitambulika wazi kwamba mkataba wake wa sasa utafikia kikomo mara baada ya msimu ujao kumalizika mwezi Mei mwaka 2012 hivyo ikitakua jukumu la uongozi wa klabu ya Schalke 04 kumuuza kwa kuhofia huenda akaondoka akiwa kama mchezaji huru.

Tayari mabingwa wa zamani wa nchini Ujerumani Bayern Munich wameshatangaza nia ya kutaka kumsajili kipa huyo ambae huenda akawagharimu kiasi cha paund million 20 kama ada ya uhamisho wake kutoka huko Veltins-Arena, mjini Gelsenkirchen.

Mbali na mabingwa hao wa zamani wa nchini Ujerumani pia imearifiwa kwamba mashetani wekundu kutoka nchini Uingereza Man Utd wanamuwania kipa huyo kwa udi na uvumba kwa ajili ya kutaka kuziba nafasi ya kipa wao wa sasa Edwin van der Sar ambae tayari ameshatangaza kustahafu soka mwishoni mwa msimu huu.

No comments:

Post a Comment