MKURUGENZI Mkuu wa klabu ya Juventus Giuseppe Marotta amekana kufanya mazungumzo na meneja wa klabu ya Manchester City Roberto Mancini.
Giuseppe Marotta amekana taarifa hizo kufuatia uvumi unaoendelea katika vyombo mbali mbali vya habari ambao unadai kwamba Roberto Mancini ambae kwa sasa ana ndoto ya kuizawadia ubingwa wa FA Man City huenda akarejea nyumbani kuinoa Juventus yenye maskani yake makuu mjini Turine.
Kiongozi huyo alisema kwamba kwa sasa bado wana mkataba na meneja wao Luigi Del Neri na katu hawezi kuzungumza lolote hadi msimu huu wa ligi utakapomalizika huko nchini Italia.
Hata hivyo wakala wa Roberto Mancini, Giorgio De Giorgis amezikana taarifa hizo huku akidai kwamba mtu wake bado ana mkataba na klabu ya Man city na yeye amekua akizisikia taarifa hizo katika vyombo vya habari.
Katika hatua nyingine Giuseppe Marotta amekanusha uvumi mwingine wa kumnyemelea meneja wa klabu ya Napoli Walter Mazzarri ambae amekiwezesha kikosi chake kuwa miongoni mwa vilabu vinavyofikiriwa kucheza ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu ujao.
No comments:
Post a Comment