KOCHA wa klabu ya Manchester City Roberto Mancini amesema endapo mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Argentina Carlos Tevez hatocheza mchezo wa ligi dhidi ya Tottenham utakaochezwa jumanne ya juma lijalo, atakua na nafasi finyu ya kucheza mchezo wa hatua ya fainali ya kombe la chama cha soka nchini Uingereza FA utakaochezwa May 14 kwenye uwanja wa Wimbley dhidi ya Stoke City.
Roberto Mancini ameanika wazi mustakabali wa mshambuliaji huyo alipokukata na waandishi wa habari hii leo huko City Of Manchester kwa ajili ya kuelezea matayarisho wa kikosi chake kabla ya mchezo wa ligi wa mwishoni mwa juma hili dhidi ya Everton watakaokua nyumbani huko Goodison Park.
Alisema mshambuliaji huyo tayarti imeshafahamika hatoweza kucheza mchezo wa mwishoni mwa juma hili na madaktari wa klabu wamemthibitishia kwamba Carlos Teves huenda akawa na nafasi ya kujumuika na wenzake katika kikosi kitakachorejea uwanjani siku ya jumannne.
Alisema kimahesahu zimesalia siku 10 kabla ya mchezo wa hatua ya fainali ya kombe la FA hivyo mshambuliaji huyo akishindwa kupita katika vipimo vya afya atakagvyofanyiwa kabla ya mchezo dhidi ya Spurs atakuwa na wakati mgumu wa kurejea uwanjani.
Carlos Tevez alipata maumivu ya nyama za paja wakati wa mchezo wa ligi dhidi ya Liverpool, hatua ambayo ilimsababishia kutolewa nje katika mchezo huo na nafasi yake kuchukuliwa na Super Mario Balotelli.
Wakati huo huo Mancini ameeleza wazi juu ya matarajio yake ya kuhakikisha wanatecheza ligi ya mabingwa barani ulaya msimu ujao ambapo alisema kimahesabu wanahitaji point nne pekee kutimiza malengo hayo.
Mancini alisema licha ya kuzitamka point hizo bado ni ngumu kupatikana kufuatia michezo inayowakabili na mchezo dhidi ya Tottenham, ameutaja kama mtihani wao mkubwa wa kutimiza malengo waliyojiwekea msimu huu.
No comments:
Post a Comment