BAADA ya kuondoshwa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya ndani ya siku tatu zilizopita, Rais wa klabu ya Real Madrid Florentino Perez ameanza kutangaza mikakati ya usajili huku chaguo lake la kwanza likiangukia kwa nahodha na kiungo wa klabu ya Arsenal ya nchini Uingereza Cesc Fabregas.
Florentino Perez ametangaza mikakati hiyo huku akitambua fika Cesc Fabregas anawani vikali na FC Barcelona waliomkuza kabl ya kumuuza jijini London kwa meneja Arsene Wenger.
Tayari raisi huyo wa klabu ay Real Madrid ameshakutana na meneja Jose Mourinho na kukubaliana taratibu za kusajili kwa Fabregas mwishoni mwa msimu huu na huenda kitita cha paund million 35 kikatumika kama ada ya uhamisho wake.
Mikakati iliyopo huko Santiago Bernabeu kwa ajili ya msimu ujao ni kuimarisha safu ya kiungo ambapo inaaminika endapo Fabregas atasajiliwa klabuni hapo ushirikiano kati yake na kiungo Xavi Alonso utaleta tija ya kupatikana kwa mafanikio na hii ni kwa mujibu wa mipango itakayotumika na Jose Mourinho msimu ujao.
No comments:
Post a Comment