KOCHA wa Manchester United Sir Alex Ferguson amewataka wachezaji wake kutowahofia mabingwa wa soka nchini Hispania Fc Barcelona ambao watakutana nao katika mchezo wa hatua ya fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya utakaochezwa May 28 katika uwanja wa Wimbley jijini London.
Ferguson ametoa rai hiyo kwa wachezaji wake ikiwa ni saa chache baada ya kumaliza shughuli ya kuwaadhibu Schalke 04 katika mchezo wa pili wa hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya mbapo wawakilishi hao wa nchini Ujerumani walikubali kisago cha mabao manne kwa moja na kupelekea kutupwa nje ya michuano hiyo kwa jumla ya mabao sita kwa moja.
Alisema jukumu zito ambalo amewabebesha wachezaji wake ni kuhakikisha wanacheza kwa kujituma na kwa kujiamini wakati wote katika mchezo huo ambao utakua na lengo la kumtoa bingwa wa michuano hiyo ya barani ulaya katika msimu wa mwaka 2010-11.
Katika hatu anyingine mzee huyo mwenye umri wa miaka 67, alitoa kauli iliyowafurahisha wengi lakini bado ikaonekana ina umuhimu mkubwa, ya kumuomba ushauri kocha wa Real Madrid Jose Mourinho kwa ajili ya kufahamu mbinu za kuifunga Fc Barcelona.
Wakati huo huo Sir Alex Ferguson amekiri kwamba katika hatua ya nusu fainali walikutana na klabu nzuri na yenye kujua namna ya kuonyesha upinzani lakini kwa uzoefu na uwezo wa wachezaji wake wamefanikiwa kuchomoza na ushindi mnene unaowapelekea fainali itakayochezwa katika ardhi ya nchini Uingereza.
Itakumbukwa kuwa Man Utd wanaelekea katika hatua ya fainali kwa mara ya nne wakiwa chini ya utawala wa Sir Alex Ferguson ambae naingia katika orodha ya mameneja waliowahi kufanya hivyo siku za nyuma wakiwa na klabu moja.
Mameneja hao ni pamoja na:
Miguel Muñoz Mozún
Real Madrid (*1959-60, 1961-62 , 1963-64 na 1965-66*,)
Marcello Lippi
Juventus (1995–96*, 1997–98 na 2002–03 )
Sir Alex Ferguson
Man Utd (1998-99*, 2007-8* 2008-9 na 2010-11 )
No comments:
Post a Comment