Saturday, May 7, 2011

FIFA KULEGEZA MASHARTI YA URAIA.

LONDON, England
SHIRIKISHO la Soka Duniani (FIFA) linatarajia kujadili suala la kupunguzwa kwa masharti ya utaifa wa mchezaji pale anapohitaji kuihama nchi yake na kulichezea taifa linguine katika michuano mbali mbali.

Wajumbe wa katia kuu ya FIFA watalijadili suala hilo katika mkutano mkuu utakaofanyika June mosi nchini Usiwz katika mji wa Nyon ambapo agenda hiyo imekua ikipigiwa upatu na mataifa mengi kutoka barani Asia.

Kubwa ambalo linafikiriwa kuzungumzwa katika agenda hiyo na kupelekea masharti kupunguzwa ya sheria hiyo ni kumuwezesha mchezaji husika alietimiza umri wa miaka 18 kuishi kwa muda wa miaka mitatu ndani ya nchi anayokusudia kuichezea hapo baadae.

Sheria hiyo kwa hivi sasa inamtaka mchezaji kufanya maamuzi ya kubadilisha uraia akiwa na umri wa miak 18 na inamlazimu kusubiri hadi miaka mitano.

Agenda nyingine katika mkutano huo wa June mosi itakua ni uchaguzi mkuu wa raiai ambapo raisi wa sasa wa FIFA Joseph Sepp Blatter atapambana vikali na raisi wa shirikisho la soka barani Ulaya Mohamed Bin Hammam kuwani kiti cha uraisi.

No comments:

Post a Comment