Wednesday, June 15, 2011

MAKONGO DAY: LEADERS KUFUKA MOTO JUMAMOSI.

JUMUIYA ya wanafunzi waliowahi kusoma na ambao wanasoma katika shule ya Secondari ya Makongo, wanatarajiwa  kufanya Bonanza la aina yake katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni Jijini Dar es Salaam..
Dhumuni la Bonanza hilo ni kuhamasisha vijana kwa wazee kuwa michezo ni ajira.,Makongo ni moja ya shule ambayo imetoa wanamichezo wengi ambao wamefanya mengi katika sekta ya michezo mbali mbali hapa nchini..
Ratiba kamili ya bonanza hilo ambalo,lifanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Leaders club watu wote wapenda michezo wataalikwa kuja kushiriki katika tamasha hilo,ambapo kiingilio kitakuwa shilingi 2000 tu kwa kila mtu..


                                                 RATIBA NI KAMA IFUATAVYO
08:00 - 09:00   Asubuhi -Wanafunzi waliosoma na walioko Makongo watajumuika kwa pamoja kufanya
                        Usafi    katika eneo lote la shule ya Makongo

09:00 - 10:00   Dua au Misa kwa ajili ya kuwaombea Walimu na Wanafunzi wote waliosoma Makongo
                         Ambao Wametutangulia mbele za haki

10:00 - 11:00   Watu wote kutoka katika Shule ya Makongo kuelekea katika Viwanja vya Leders Club
                        Kujumuika kwa pamoja na wadau na wapenzi wa michezo hapa Nchini

11:00 - 14 : 00 Michezo mbali mbali kuanza,kwa wanafunzi wote, waliosoma na wanaoendelea kusoma
                        Katika shule ya Makongo pamoja na wadau wa michezo kujumuika kwa pamoja..

14:00 - 14 :30 Lisala kwa wanafunzi kwenda Waalimu na Uongozi wa Shule na Lisala kwa wanafunzi wa
                       Zamani kwenda walimu na wanafunzi wa sasa.

16:00 - 18:00  Mechi kati ya wanafunzi wa Makongo na Timu ya Yanga

18:00 -  00:00 Burudani Kutoka kwa Tmk Wanaume,Chege Na Temba,Mapacha wa Tatu,Dogo Janja na
                       Tip Top Connection,Na wengine wengi Kutoka Makongo..

No comments:

Post a Comment