RAIS wa klabu ya Udinese Giampaolo Pozzo amekanusha taarifa zilizotolewa mapema hii leo ambazo zilidai kwamba wamekubali kumuuza mshambuliaji wa pembeni Alexis Sanchez kunako klabu ya Fc Barcelona.
Pozzo alisema taarifa hizo zimewashangaza wao kama viongozi wa klabu hiyo inayomshikilia mchezaji huyo na pia akaendelea kusisitiza kuwa Sanchez bado yupo sokoni katika kipindi hiki.
Alisema wengi wamekua na lengo baya na klabu yake na huenda baadhi ya watu wamediriki kutoa habari hizo za kizushi ambazo alisema bado hazijawachafua kwani mshambuliaji huyo wa pembeni ni mali yao.
Taarifa zilizotolewa kwenye mitandao mbali mbali zilidai kwamba mabingwa wa soka barani Ulaya Barcelona wamekubalai kumsajili Sanchez kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 33 sambamba na kumtoa kinda Fernando Felicevich.
Kwa muda wa majuma kadhaa sasa Sanchez amekua akihusishwa na taarifa za kutaka kusajiliwa na klabu za Manchester United, Manchester City, Chelsea, Barcelona, Inter Milan pamoja na Juventus.
No comments:
Post a Comment