Tuesday, June 21, 2011

MARADONA AKERWA NA VYOMBO VYA HABARI KUKUZA HABARI ZA KUHAMA MKWEWE.

MADRID, Hispania
GWIJI wa soka nchini Argentina Diego Maradona amekereka na taarifa zinazomuhusisha mkwewe Sergio Aguero za kutaka kujiunga na klabu ya Chelsea ya Uingereza ama Juventus ya nchini Italia.

Maradona alisema taarifa hizo ambazo zimekua zikitolewa kila leo na vyombo vya habari zinamkera na hapendezwi nazo kufuatia mikakati iliyowekwa na mkwewe ya kutaka kuendelea kucheza soka nchini Hispania.

Alisema Aguero alieleweka vibaya alipotamka yu tayari kuondoka Atletico Madrid kwa ajili ya kubadili mazingira ya soka lake na ndipo wengi walipodhani huenda akawa na mipango ya kuelekea Chelsea ama Juventus katika kipindi hiki.


Maradona amebainishwa kwamba mshambuliaji huyo hakumaanisha kwa namna ya alivyonukuliwa na vyombo vya habari bali alimaanisha anataka kupata changamoto mpya akiwa ndani ya jiji la Madrid hivyo endapo atapata nafasi ya kujiunga na Real Madrid atakua tayari kufanya hivyo.

Aguero ni baba wa mtoto mmoja aitwae Benjamín ambae amezaa na mtoto wa Maradona Giannina mara baada ya kufunga ndoa 19 February 2009.

No comments:

Post a Comment