KOCHA wa klabu ya National Al-Ahly ya nchini Misri Manuel Jose, anafikiriwa kupewa jukumu la kuwa Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya nchi hiyo ambayo imepoteza muelekeo wa kutetea ubingwa wa barani Afrika katika fainali zijazo.
Jose anafikiriwa kupewa jukumu hilo kufuatia hatua ya kujiuzulu kwa aliekua kocha wa timu ya taifa ya Misri Hassan Shehata siku chache baada ya kikosi cha The Pharaohs kupata matokeo ya sare ya bila kufungana dhidi ya timu ya taifa ya Afrika Kusini.
Hata hivyo bado mazungumzo kati ya viongozi wa Shirikisho la Soka nchini Misri dhidi ya viongozi wa klabu ya Al-Ahly hayajaanza kufanywa licha ya taarifa hizo kufahamika mapema.
Endapo dili la Jose litakamilika mipango atakayokua nayo ni kuhakikisha timu ya taifa ya Misri inacheza fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2014 zitakazounguruma nchini Brazil.
No comments:
Post a Comment