Wednesday, June 22, 2011

BARCA YASUBIRI HURUMA YA ARSENAL ILI WAMCHUKUE FABREGAS.

BARCELONA, Hispania
RAIS wa klabu bingwa nchini Hispania pamoja na barani Ulaya kwa ujumla FC Barcelona Sandro Rosell alisema klabu yake ipo tayari kutoa kiasi cha paund million 35 kama ada ya uhamisho wa nahodha na kiungo wa klabu ya Arsenal Cesc Fabregas.

Rosell, ametoa kauli hiyo kufautia uongozi wa klabu ya Arsenal kushikilia msimamo wa kuwa tayari kumtoa Cesc Fabregas kwa ada ya uhamisho wa paund million 40 ambayo toka msimu uliopita imekua ikitajwa na viongozi wa klabu hiyo ya Emirates.


Rosell alisema kimtazamo na kimahesabu hawawezi kukubali kutoa zaidi ya paund million 35, kwani mara kadhaa wamekua wakipata ushauri kutoka kwa meneja wa kikosi chao Josep Pep Guardiola Isala ambapo amesema Fabregas, hana thamani ya paund million 40 zinazotakiwa na uongozi wa Arsenal.

Mpango huo wa klabu ya Barclona umeibuliwa na Sandro Rosell, huku taarifa zikieleza kwamba pamekuwepo na mawasiliano kati yake na mwenyekiti wa klabu ya Arsenal Peter Hill-Wood kwa ajili ya kufunguliwa milango ya mazungumzo ya kuuzwa kwa Fabregas katika kipindi hiki.


Katika hatua nyingine Rosell, alisema bado hawajakamilisha usajili wa mshambuliaji wa pembeni wa klabu ya Udanise ya nchini Italia Alexis Sanches kama ilivyoriopotiwa mapema jana na badala yake wanaendelea na mipango hiyo.

Taarifa zilizotolewa mapema hiyo jana zilieleza kwamba FC Barcelona wamekubali kutoa ada ya uhamisho wa paund million 33 baada ya kukamilika kwa mazungumzo kati yao na viongozi Udanise.

Wakati huo huo Rais huyo wa Barcelona alisema bado hawajapokea taarifa zozote kutoka kwa mahasimu wao wakubwa Real Madrid zinazomuhusu beki wa pembeni Eric Abidal ambae amegoma kusaini mkataba mpya.

Eric Abidal amegoma kusaini mkataba mpya huku ikielezwa kwamba huenda jeuri ya kufanya hivyo ameipata kufautia ukaribu uliopo kati yake na Rais wa klabu ya Real Madrid Florentino Perez ambae bado ana mipango ya kuendelea kukisuka kikosi cha klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment