UONGOZI wa klabu ya Aston Villa umemtambulisha rasmi kocha mpya wa klabu hiyo Alex McLeish kwa waandishi wa habari baada ya kumtangaza kushika wadhifa huo mwishoni mwa juma lililopita huko Villa Park.
Uongozi wa klabu hiyo umefanya hivyo huku ukitambua fika asilimia kubwa ya mashabiki wa The Villans hawakufurahishwa na hatua ya McLeish kupewa ajira klabuni hapo huku ikiaminiwa kwamba huenda kocha huyo wa nchini Scotland akashindwa kufanya vizuri kama ilivyokua kwa mahasimu wao Birmingham City.
Hata hivyo katika utambulisho huo McLeish ameomba kupewa muda na ana imani atafanya vyema na kila kitu kitakua vizuri klabuni hapo licha ya kuwepo kwa imani pungufu dhidi yake.
Amewataka mashabiki wa Aston Villa kumpa ushirikiano wa kutosha katika kipindi hiki cha maandalizi ya msimu ujao wa ligi na endapo hatua hiyo itatekelezwa ipasavyo basi kuna kila sababu ya mipango ya kufanya vizuri.
McLeish ametangazwa kuwa kocha mpya wa klabu ya Aston Villa baada ya kuondoka kwa aliekua kocha klabuni hapo msimu uliopita Gerard Houllier kufuatia hali yake ya kiafya kutokua nzuri.
No comments:
Post a Comment