Tuesday, June 28, 2011

MUNTARI AIFAGILIA ASANTE KOTOKO.

ACCRA, Ghana
KIUNGO wa kutoka Ghana Sulley Muntari amesema endapo itatokea nafasi ya kurudi nyumbani kwao kucheza soka atakua tayari kuitumikia klabu ya Asante Kotoko na si klabu nyingine yoyote.

Muntari ametoa msimamo huo kufautai sakata lake la uhamisho linaloendelea kupewa nafasi katika vyombo mbali mbali vya habari nchini Ghana ambapo taarifa zasema kwamba klabu yake ya Inter Milan ya nchini Italia ipo mbioni kumuuza katika kipindi hiki.

Akizungumza na kituo cha televisheni ya TV3 mjini Kumasi mapema hii leo kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26 alisema anaithamini na kuipenda klabu ya Asante Kotoko licha ya historia yake kuonyesha kwamba alilelewa na klabu ya Liberty Professionals ya mjini Accra.

Alisema Asante Kotoko ina mipango mzuri ambayo hujionyesha kila msimu unapowadia na anaamini hatua hiyo inawasadia kwa kiasi kikubwa wachezaji wa klabu hiyo ya mjini Kumasi.

Katika sakata la usajili wa mchezaji huyo linaloendelea barani ulaya Muntari bado anaendelea kuhusishwa na taarifa za kuwa mbioni kuuzwa na klabu ya Inter Milan katika kipindi hiki cha usajili na klabu inayotajwa sana kuwa tayari kufanya hivyo ni Garatasalay ya nchini Uturuki.

Kama itakumbukwa uzuri hapo jana Muntari alisema kwamba yu tayari kuondoka Inter Milan kwa mkopo kama ilivyokua msimu uliopita ambao ulishuhudia akirejea nchini Uingereza kuitumikia Sunderland kwa mkopo.

No comments:

Post a Comment