Tuesday, June 28, 2011

RODRIQUEZ ATIMKIA MALAGA.

MALAGA, Hispania
UONGOZI wa klabu ya Malaga ya nchini Hispania umekubali kumsajili kiungo wa nchini humo pamoja na klabu ya Valencia Joaquín Sánchez Rodríguez.

Uongozi wa klabu ya Malaga Umekubali Kumsajili Kiungo huyo Mwenye Umri wa Miaka 29, baada ya kukamilika kwa mazungumzo yalioyodumu kwa siku nne zilizopita.

Sehemu ya makubalia ya pande hizo mbili ni pamoja na kutotajwa kwa kiasi cha fedha kitakachotumika kama sehemu ya ada ya uhamisho wa Joaquín Sánchez Rodríguez ambae alijiunga na Valencia mwezi August mwaka 2006 akitokea Real Betis kwa ada ya uhamisho wa paund million 22.

Hata hivyo licha ya makubaliano hayo kufikiwa, baadhi ya vyombo vya habari nchini Hispania vimeripoti kwamba uhamisho wa Joaquín Sánchez Rodríguez, utaigharimu Malaga kiasi cha Euro million tano.

Kwa mantiki hiyo sasa Joaquín Sánchez Rodríguez anajiunga na wachezaji wengine ambao tayari wameshasajiliwa na klabu ya Malaga iliyo chini ya mmiliki kutoka nchini Qatar, ambao ni Diego Buonanotte, Martin Demichelis, Joris Mathijsen, Ruud van Nistelrooy pamoja na Nacho Monreal.

No comments:

Post a Comment