GIAN Piero Gasperini, ametajwa kuwa kocha mpya wa klabu ya Inter Milan.
Gasperini ametangazwa kushika wadhifa huo huko Stadio Giuseppe Meazza, baada ya kuondoka kwa aliekua kocha Leonardo Nascimento de Araújo ambae anahusishwa na taarifa za kupewa kibarua huko nchini Ufaransa katika klabu ya PSG kama Mkurugenzi wa Ufundi.
Gasperini, anarejea katika utawala wa soka nchini Italia baada ya kutimuliwa kazi mwezi November huko Stadio Luigi Ferraris, yalipo makuu ya klabu ya Genoa ambapo mkasa huo ulimkuta kufuatai matokeo mabovu yaliyokua yakimuandama.
Hata hivyo uongozi wa Inter Milan ulikua na mipango ya kutaka kumpa kibarua aliewahi kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Argentina kuanzia 1998–2004 Marcelo Bielsa lakini hatua hiyo ilishindikana baada ya mlengwa kugoma kusaini mkataba aliopewa.
Mbali na kocha huyo kutoka nchini Argentina, Inter Milan walikua na mipango mingine ya kutaka kumchukua meneja wa sasa wa klabu ya Chelsea Villas-Boas lakini masharti waliyowekewa na viongozi wa Fc Porto yalikua kikwazo.
No comments:
Post a Comment