Tuesday, June 28, 2011

WOLFBURG YAMTEMA DIEGO.

WOLFBURG, Ujerumani
KIUNGO kutoka Brazil Diego Ribas da Cunha, amefunguliwa mlango wa kutokea huko Volkswagen Arena yalipo Makao Makuu ya klabu ya VfL Wolfsburg kufautia kutowepo katika mipango ya kocha alierejea kundini Wolfgang-Felix Magath.

Diego ambae alijiunga na Wolfsburg mwaka 2009 akitokea Juventus ya nchini Italia, amepewa taarifa za kuondoka klabuni hapo huku akiwa bado ana mkataba hadi mwaka 2014.

Taarifa za kutokuwepo kwenye mipango ya Magath zinahusishwa na matatizo yaliyojitokeza mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kiungo huyo kuachwa nje ya kikosi katika moja ya michezo ya mwishoni mwa msimu.

Hata hivyo uongozi wa Wolfsburg umempa Diego nafasi ya kuendelea kufanya mazoezi na wachezaji wenzake wakati wa kujiandaa na msimu mpaka hapo atakapopata klabu ya kuitumikia kwa ajili ya msimu ujao.

No comments:

Post a Comment