Wednesday, June 15, 2011

ST ETIENNE YAMWEKA SOKONI MATUIDI.

PARIS, Ufaransa
UONGOZI wa klabu ya St Etienne umetangaza dau la kumuuza kiungo wa kimataifa toka nchini humo Blaise Matuidi ambae anatakiwa kwa udi na uvumba huko Parc des Princes yalipo makao makuu ya klabu ya PSG.

Uongozi wa klabu hiyo umetangaza dau la paundi million 13.2 (€15m) ambalo litatumika kama ada ya uhamisho wa mchezaji huyo kwa klabu yoyote itakayo hitaji kumsajili katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye msimu wa mwaka 2011-12.

Hata hivyo uongozi wa PSG tayari umeshaonyesha nia ya kuwa tayari kutoa pesa hizi kufuatia pesa za usajili zilizotengwa na wamiliki wa klabu hiyo kutoka nchini Qatar Kevin Gameiro pamoja na Nicolas Douchez.

No comments:

Post a Comment