KOCHA wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amemtahadharisha kiungo wake Samir Nasri juu ya mipango aliyo nayo na kutaka kuondoka huko Ashburton Grove na kujiunga na klabu ya Manchester United ambayo tayari imeshaonyesha dalili zote za kutaka kumsajili katika kipindi hiki.
Wenger amemueleza Nasri kwamba bado ana kila sababu za kuendelea kuwepo katika himaya ya Arsenal kufuatia muda wake wa kuondoka klabuni hapo kutotimia kama ilivyo kwa wachezaji wengine walioamua kuondoka.
Wenger alisema kuna uwezekano mkubwa kwa Nasri akajutia maamuzi atakayoyafanya kama ilivyokua kwa wachezaji wengine ambao walijiona wameiva na mwishowe wameishia katika majuto ya kila siku ya kuondoka Emirates.
Hata hivyo mzee huyo wa kifaransa amedai kwamba bado wanaendelea na mipango ya kuhakikisha kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 anaendelea kubaki klabuni hapo kwa ajili ya kutaka kutimiza malengo waliyojiwekea ya kusaka mafanikio baada ya kukosa ubingwa katika msimu wa mwaka 2010-11.
Katika hatua nyingine kibopa wa kimarekani Stane Kroanke ameahidi kufanya jitihada binafsi za kuhakikisha wachezaji wote wanaohusishwa na taarifa za kutaka kuondoka klabuni hapo, hawafanyi hivyo kama inavyodaiwa.
Stane Kroanke ambae kwa sasa ndie mwenye sauti ndani wa klabu ya Arsenal amesema hakuna kinacho shindikana zaidi ya kukaa chini na wahusika na kuwaeleza wazi mipango iliyopo ndani ya Arsenal ya sasa na ya baadae ambayo inatabiriwa kuwa na mafanikio zaidi.
Wachezaji walio mbioni kuondoka Arsenal ni Nasri anaewaniwa na klabu ya Man United, Bayen Munich pamoja na Inter Milan, Cesc Fabregas anaesemekana huenda akarejea nyumbani kwao Barcelona kujiunga na mabingwa wa soka nchini Hispania FC Barcelona pamoja na Gael Clich alie mbioni kujiunga na klabu ya Liverpool.
No comments:
Post a Comment