Friday, July 15, 2011

MESSI: NI MAKOSA KUIFANISHA ARGENTINA NA BARCELONA.

CORDOBA, Argentina.
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Argentina na klabu ya Barcelona Leonel Messi amedai kwamba haina maana yoyote kuifananisha timu yake ya Taifa na klabu yake.

Ujumbe wake huo umekuja ikiwa ni siku moja baada ya kuandamwa kuwa anacheza chini ya kiwango awapo timu ya taifa tofauti na anavyocheza katika klabu yake.

Lakini Messi alifafanua sababu za kwanini awapo klabuni anacheza kwa kiwango cha juu ukilinganisha na awapo timu ya taifa.

"Kuifananisha Argentina na Barcelona ni makosa," Alisema Messi akihojiwa na katika mkutano wa waandishi juu ya mchezo wao wa robo fainali ya michuano ya Copa America Jumamosi dhidi ya Uruguay.

"Tunafanya kazi kwa muda mrefu tukiwa Barcelona, wakati katika timu ya taifa tunajaribu kufanya vitu vinavyofanana. Hatahivyo huwezi kufananisha timu hizo mbili," alisema Messi.

"Mchezo dhidi ya uruguay utakuwa nimgumu, lakini ndoto zetu ni kushinda mashindano hayo," alisema Messi.

"Tunahitaji kunyakuwa kombe la Copa America kama Argentina inavyohitaji taji na tunalifanyia kazi hili."

No comments:

Post a Comment