Friday, July 15, 2011

BOATENG ATUA RASMI BAYERN.

MUNICH, Ujerumani
BEKI wa Bayern Munich Jerome Boateng amefurahishwa sana na jinsi uhamisho wake kutoka Manchester City ulivyokamilika.

Boateng (22) yuko Munich kumalizia uhamisho wake baada ya Bayern kutangaza kuwa wamekubaliana na Man City kuhusu uhamisho huo Alhamisi.

Boateng anaishukuru Bayern kwa kazi kubwa walioifanya baada ya vuta nikuvute kuhusu ada ambayo mpaka sasa haijawekwa wazi.

"Sasa nina furaha isiyo na kifani hili suala limekwisha salama na nashukuru klabu haikukata tamaa pamoja na mazungumzo kuhusu kuuzwa kwangu kuwa magumu."

Beki huyo wa kimataifa wa Ujerumani anarajiwa kusaini mkataba wa miaka minne pindi atapomaliza vipimo vyake vya afya.

No comments:

Post a Comment