Saturday, July 16, 2011

UHAMISHO WA WACHEZAJI 2011/12.

DAR ES SALAAM, Tanzania
UHAMISHO wa wachezaji wa Ligi Kuu kwa msimu wa 2011/2012 ulifikia tamati jana saa 6 kamili usiku.Wachezaji ambao maombi yao ya uhamisho yamewasilishwa TFF ni Shabani Kado kutoka Mtibwa Sugar kwenda Yanga, Salum Machaku kutoka Mtibwa Sugar kwenda Simba na Idrisa Rajab kutoka African Lyon kwenda Yanga.

Hao ni kwa wachezaji ambao maombi yao yametumwa kwa njia ya barua. Kwa vile uhamisho vile vile unaweza kufanywa kwa njia ya mtandao (Transfer Match System-TMS), uhamisho mwingine uliofanyika utafahamika kesho baada ya Kurugenzi ya Mashindano kupitia mfumo huo wa TMS ambao klabu zote za Ligi Kuu tayari zina namba zao maalumu za kuingia (passwords).

WACHEZAJI WALIOTOLEWA KWA MKOPO
Wachezaji waliotolewa kwa mkopo kutoka Simba kwenda klabu zingine ni Aziz Gilla na Mbwana Bakari (Coastal Union), Mohamed Kijuso, Mohamed Banka na Haruna Shamte (Villa Squad), Meshack Abel (Ruvu Shooting), Juma Jabu, Andrew Kazembe, Paulo Terry na Godfrey Wambura (Moro United).

Kutoka Azam ni Sino Augustino na Selemani Kassim ambao wanakwenda African Lyon,na Tumba Louis (Moro United). Yanga imewapeleka wachezaji wake Omega Seme na Idd Mbaga kwa mkopo African Lyon.

MORO UNITED KUCHEZA CHAMAZI
Klabu ya Moro United imewasilisha barua ya kutumia Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom. Nayo Villa Squad imeomba kutumia uwanja huo huo, ingawa bado haijaonesha barua kutoka Azam inayowaruhusu kutumia uwanja wao.

Klabu ya African Lyon ndiyo pekee ambayo bado haijawasilisha uwanja ambao itautumia kwa ajili ya ligi hiyo itakayoanza Agosti 20 mwaka huu. Kwa Lyon kushindwa kuleta jina la uwanja wake hadi sasa inasababisha TFF kuchelewa kutoa ratiba ya ligi, hivyo tunaitaka Lyon kutimiza wajibu wake katika suala hilo haraka.

No comments:

Post a Comment