Monday, July 11, 2011

TIMU YA MEXICO UNDER 17 YANYAKUWA KOMBE LA DUNIA.

MEXICO CITY, Mexico
WENYEJI Mexico jana walitawadhwa mabingwa wapya wa Kombe la Dunia la Vijana chini ya Umri wa Miaka 17 baada ya kuifunga Uruguay mabao 2-0 katika mchezo wa fainali ulifanyika Mexico City.

Mexico walipata bao la kuongoza dakika ya 31 kupitia kwa mshambuliaji wake Antonio Briseno na Giovan Casillas alipigilia msumari wa mwisho dakika za majeruhi na kuihakikishia timu yake ushindi.

Mafanikio hayo ni ya pili kwa timu hiyo ya Mexico chini ya miaka 17 kutwaa ubingwa yakifuatiwa na yale ya mwaka 2005 nchini Peru.

Mexico pia walishinda michuano ya Gold Cup kwa wakubwa na kuendeleza kipindi cha mafanikio katika soka katika taifa lililopo Kaskazini mwa Amerika.

No comments:

Post a Comment