Thursday, August 4, 2011

FERGUSON: BERBATOV RUKSA KUONDOKA.

LONDON, England
MIAKA ya kuhangaika kufanya vizuri ndani ya United kwa Dimitar Berbatov inaonekana kuelekea mwishoni baada ya jana Sir Alex Ferguson kukiri kuwa mbulgaria huyo anaweza kujiunga na Paris Saint Germain.

Klabu mpya tajiri ya Ufaransa wamekuwa wakimtaka Berbatov kipindi hiki chote cha usajili na hatimaye wamefanya mawasiliano na Red Devils.

Akiulizwa kupitia French TV baada ya kikosi cha United XI kufungwa na Mersaile 8-2 mjini Monaco kama Dimitar anaweza kwenda Ufaransa, United Manager alisema: “Ndio, anaweza.Hilo linawezekana.”

No comments:

Post a Comment