MSHAMBULIAJI wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amesisitiza kuwa timu yake haihitaji kusajili mshambuliaji mwingine katika kipindi hiki cha kiangazi.
Timu hiyo inayonolewa na Jose Mourinho imekuwa ikihusishwa na suala la kusajili washambuliaji mbalimbali akiwemo mshambualiaji wa Santos Neymar na Emmanuel Adebayor wa Manchester City lakini Ronaldo anaona washambualiji waliopo wanatosha.
"Hatuhitaji kusajili mshambualiaji mwingine. Nafikiri inabidi tujivunie kikosi tulichonacho sasa," alisema Ronaldo akihojiwa na luninga ya ESPN.
Madrid tayari wameshapata saini ya Jose callejon kutoka Espanyol ilikuongeza nguvu katika ushambualiaji lakini Mourinho anaonekana hajatosheka pamoja na comments iliyotolewa na Ronaldo na anahitaji kuongeza mshambuliaji mwingine.
No comments:
Post a Comment