Monday, August 1, 2011

SANTOS YATISHIA KUISHTAKI MADRID KUHUSU NEYMAR.

SANTOS, BRAZIL
MABINGWA wa Copa Libertadores Santos wamedhamiria kuendelea kuwa na mchezaji wao Neymar mpaka yatakapomalizika michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia, lakini klabu ya Real Madrid wameamua kumfungia kibwebwe mchezaji huyo kwa kuweka kitita cha Euro milioni 45 mezani na tayari wameshaanza mazungumzo na wakala wa mchezaji huyo kuhusu kumyakua mchezaji huyo.

"Kama Madrid au klabu nyinginye yeyote ambao watakutana na mchezaji huyo kwa nia ya kumnunua hatutakuwa na njia nyingine bali ni kuwashitaki kwa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kwa kuongea na mchhezaji bila ridhaa yetu. Mjadala kuhusu mchezaji huyo umefungwa na hautafunguliwa kwa sasa," alisema mmoja wa viongozi wa klabu hiyo.

"Real Madrid walishaongea na wakala wa Neymar jijini Paris na kuweka dau zuri. Nilishamwambia hatutamwachia aende hatahivyo na yeye anahitaji kuwa nasi pia.

"Nataka nikuhakikishie kuwa Neymar ataichezea Santos michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia. Nilishasema hivyo kabla na ndivyo itakavyokuwa."

Mkataba wa Neymar (19) katika klabu ya Santos unakwisha 2015.

No comments:

Post a Comment