KOCHA wa Arsenal Arsene Wenger amekiri kuwa anahitaji kuongeza nguvu katika kikosi kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu nchini humo.
Mashabiki wa Arsenal wamekuwa wakijipa matumaini kuhusu kutimka kwa nahodha wa timu hiyo Cesc Fabregas kwenda Barcelona wakati pia wameshashuhudia beki wake wakutegemewa akitimkia Manchester City katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi.
Mpaka sasa Wenger amekwisha wasainisha beki kinda wa kati Carl Jenkinson na mshambualiaji Gervinho lakini anaamini kuwa bado anahitaji kuongeza nguvu zaidi.
Baada ya kukiona kikosi chake kikitoa sare ya bao 1-1 na New York Red Bulls katika Kombe la Emirates Wenger alisema akihojiwa kuwa atajaribu kuongeza nguvu katika kikosi chake ingawa hakuwa tayari kutaja majina ya wachezaji anaowahitaji.
Inawezekana katika kuongeza nguvu katika kikosi cha asiongeze mabeki wa kati kutokana na kufurahishwa na jinsi mabeki wake wa kati Thomas Vermaelen na Laurent Koscielny walivyokuwa wakielewana vyema dhidi ya timu ya Redbulls.
"Nafikiri mabeki wa kati ni wazuri, kwa mawazo yangu na walicheza vizuri. kama ukiangalia goli tulilofungwa leo halikutokana na makosa ya mabeki wa kati," alisema Wenger.
"Nimefurahishwa na siku hizi mbili. Tumefanya majaribio na kwa siku hizo mbili tumecheza vizuri."
No comments:
Post a Comment