KLABU ya AC Milan imeshakamilisha uhamisho wa Robinho kutoka Manchester City kwa mkataba wa miaka minne, ilisema taarifa ya klabu kupitia mtandao wake.
"AC Milan walifanya mazungumzo kumhusu mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil, juu ya uwezekano wake wa kuhama City. Mbrazili huyo alitia saini katika klabu maarufu kama Rossoneri kwa miaka mnne" ilisomeka taarifa hiyo.
Mchezaji huyo alifaulu vipimo vya afya na klabu italipa erou milioni 18 kupata huduma yake, ingawa kiasi cha uhamisho huo kilikuwa hakijafungwa wakati taarifa hii inatoka.
Robinho hakuwa na nafasi katika kikosi cha City msimu uliopita, ndio maana alikubali kwenda kucheza kwa mkopo nyumbani kwao Brazil katika klabu ya Santos.
Sky Sport ilimnukuu mchezaji huyo akisema "Mimi sasa ni mchezaji wa Milan," akiwathibitishia wakazi wa San Siro.
Robinho atajiunga na wachezaji wenzake Ronaldinho, Zlatan Ibrahimovic na Alexandre Pato kuunda safu ya ushambuliaji itakayotisha msimu huu.
No comments:
Post a Comment