Wednesday, September 1, 2010

ZIDANE ATEMBELEA KAMBI YA UFARANSA.

MCHEZAJI nguli wa zamani wa Ufaransa Zinedine Zidane ameitembelea kambi ya timu ambayo iko katika mazoezi kwa ajili ya mchezo wake wa kusaka tiketi ya michuano ya Ulaya dhidi ya Belarus, Ijumaa hii.


Timu hiyo haikufanya vizuri katika fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika Afrika Kusini ambapo walitolewa katika hatua ya makundi, na hivi sasa wapo tayari kuanza upya chini ya kocha mpya Laurent Blanc.

Zidane alitembelea kambi hiyo kumsaidia Blanc kuiongezea timu hiyo hali ya kujiamini zaidi na kuwapa moyo wachezaji.

"Nawatakia kila la heri katika mchezo wao unaokuja." "Ni wachezaji wa kizazi kipya ambao wana majukumu muhimu ya kutekeleza mbele yao. Timu ya Ufaransa ni timu ambayo iko juu siku zote" alisema Zidane.

"Niliwaeleza umuhimu wa wao kuanza kushinda mechi wanazocheza tena kwa sababu timu nzuri huwa inapimwa kwa matokeo yake" aliongeza Zidane.

Zidane attended the training camp at Clairefontaine to help Blanc restore confidence in the France squad and inspire them.

Mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Juventus na Real Madrid pia ana imani na Blanc kwamba atafanikiwa kutokana na aina ya wachezaji alionao.

"Laurent ndiye mtu anayefaa kwa kazi hii kwa sababu ya uzoefu wake alipokuwa mchezaji. Kwasababu timu inaanzia chini, watafanya vitu vizuri wakiwa pamoja.

No comments:

Post a Comment