Wednesday, September 1, 2010

KOCHA 'BLACK STARS' AMKINGIA KIFUA ESSIEN.

UAMUZI wa mchezaji wa kimataifa wa Ghana Michael Essien kujiondoa kwa muda kuchezea timu ya Taifa ili kuelekeza nguvu katika klabu yake ya Chelsea umepokewa vizuri na kocha wa timu ya Taifa ya nchi hiyo "Black Stars" Milovan Rajevac.


"Kama ujuavyo Michael alipata maumivu mara mbili wakati akiitumikia timu ya Taifa katika miaka miwili iliyopita, hilo limemchanganya sana" alisema Mserbia huyo.

"Michael mwenyewe aliwasiliana na mimi baada ya kutaja kikosi kitakachopambana na Swaziland na kuniomba ruhusa ya kumuacha kwa muda. Najua maamuzi haya hakufanya mwenyewe. Nimemuelewa na pia nahitaji kumsaidia arudi katika kiwango chake kama zamani na nimempa hiyo ruhusa.

Naamini atarejea katika timu ya Taifa mapema mwaka ujao na pia wakati ambao tutamuhitaji zaidi" Aliongezea Rajevac

No comments:

Post a Comment