Wednesday, September 1, 2010

VUVUZELA MARUFUKU ULAYA.

SHIRIKISHO la Soka la Ulaya (UEFA) wamepiga marufuku matumizi ya vuvuzela katika michezo yake itakayoandaa.


Kifaa hicho cha vuvuzela ambacho kilikuwa kikilalamikiwa na wachezaji wengi wa Ulaya katika fainali za Kombe la Dunia zilizifanyika Afrika Kusini Juni mwaka huu hakitaruhusiwa katika mechi za Klabu Bingwa (Champions League), michuano ligi ya vilabu vya Ulaya (Europa League) na katika mechi za kutafuta tiketi ya michuano ya ulaya (Euro 2012).

Wanachama 53 waliopinga matumizi ya vuvuzela walitoa sababu kuwa wamekipiga marufuku kifaa hicho kwa kuwa hakiendani na utamaduni wa soka la ulaya huku wakikubali ushangilianji wa kuimba nyimbo na kupiga makelele mengine wawapo uwanjani.

Taarifa iliyotolewa na UEFA kupitia mtandao ilisema kuwa Kombe la Dunia lilitambulika kwa kelele za vuvuzela na kifaa hicho kitaendelea kutumika katika michuano hiyo.

"Kwa jinsi ilivyokuwa Afrika Kusini sauti ya vuvuzela ilikuwa ni kama wimbo wa nyumbani, hivyo UEFA wanaona kwamba matumizi ya vuvuzela hayatafaa kwa ulaya".

Ili kuondoa matatizo yoyote yanayoweza kujitokeza wakati mashindano ya UEFA yanapochezwa na kulinda mila na tamaduni za soka la ulaya ambapo mashabiki huimba na kushangilia wawapo uwanjani ndio maana wakaamua kukataza matumizi ya vuvuzela mara moja.

No comments:

Post a Comment