MCHEZAJI nyota wa zamani wa Argentina, Francisco Varallo ambaye ni mchezaji pekee aliyebakia kati ya wachezaji ambao walicheza Kombe la Dunia la kwanza mwaka 1930 amefariki dunia Jumatatu iliyopita nyumbani kwake Buenos Aires akiwa na miaka 100.
Varallo alikuwa ndio mchezaji mdogo zaidi katika kikosi cha Argentina kilichopoteza mchezo wa fainali dhidi ya Uruguay ambao ndio walikuwa wenyeji wa michuano hiyo kwa mabao 4-2, mchezo uliochezwa July 30, 1930 katika Uwanja wa Montevideo Centenario.
Kama mashbiki walivyozoea kumuita "The little cannon" amewahi kufunga magoli 194 akiwa na klabu maarufu ya nchini kwao Boca Juniors. Mwaka uliopita alitajwa kama mchezaji mahiri katika kipindi chake na mshambuliaji mkongwe wa nchi hiyo Martin Palemo.
"Nakumbuka vizuri mchezo ule wa fainali dhidi ya Uruguay, ambao ndio ulionifanya nijulikane mpaka leo hii" alisema Varallo wakati wa sherehe yake ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka 100, Februali mwaka huu. "Tulikuwa na timu nzuri lakini baadhi ya wachezaji hawakucheza vizuri kipindi cha pili na tukapoteza mchezo huo."
"Kila mtu ananiuliza kuhusiana na mchezo huo, ambao sikutakiwa kucheza kwa kuwa nilikuwa mdogo na nilikuwa sina uzoefu wa kutosha. muda mwingine huwa sipendi kukumbuka kilichotokea Montevideo," aliongeza Varallo.
No comments:
Post a Comment