Thursday, September 2, 2010

HISPANIA INAWEZA KUWA TIMU BORA YA KARNE - FIFA.

MAOFISA wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) wamependekeza timu ya Hispania kuwa ndio timu bora ya karne baada ya uchambuzi wao wa Kombe la Dunia 2010 lililofanyika Afrika Kusini.


Timu hiyo ilishinda Kombe hilo kwa aina ya kipekee katika ardhi ya Afrika Julai wakiongezea ubingwa Ulaya waliopata miaka miwili iliyopita. Maofisa hao wachambuzi wa soka kutoka FIFA wamesema kwamba Hispania inaweza kuwa timu bora katika historia ya soka.

Jean-Paul Brigger, Mkurugenzi wa Kamati ya Ufundi ya FIFA ambaye ni mmoja wa kundi la watu 16 ambao walitoa ripoti hiyo, alikaririwa akisema kuwa Hispania wameshinda Kombe la Ulaya 2008 na sasa ndio mabingwa wa dunia, kitu ambacho ni mafanikio ya kipekee.

"Kikosi chao kimekuwa na kuendelea pamoja na sasa wana uwezo wa kucheza vizuri na katika hali ya kuvutia."

"Wanacheza kwa uelewano na wanakimbia sana. Xavi, Iniesta na Xabi Alonso wakiwa viungo wanamiliki sehemu kubwa ya uwanja lakini wakicheza mchezo wa kuvutia na kuvutia kuutizama, lakini nakiri wanafanya kazi kubwa"

"Wana timu iliyokamilika, ambayo inaweza kuwa timu ya karne. Na mpaka katika fainali, Ujerumani nao walicheza mcheza mchezo mzuri."

Ripoti hiyo pia ilisema kuwa timu za Afrika zilipoteza nafasi za kusonga mbele katika michuano hiyo kwa kuajiri makocha kutoka nje na kulaumu magolikipa kwa makosa ambayo si ya kwao lakini ripoti hiyo haikuzungumzia kuhusu kuhusu maamuzi ya kushangaza walitoa waamuzi waliochezesha michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment