MADRID, Hispania
JOSE Mourinho amesema amesikitika kuwakosa washambuliaji nyota Didier Drogba wa Chelsea na Emmanuel Adebayor kutoka Manchester City majira ya kiangazi.
Kocha huyo aliyeipa ubingwa wa Ulaya Inter Milan, alisema baada ya kujiunga Real Madrid, alitaka kumsajili mshambuliaji wa katina alimpa nafasi kubwa rafiki yake Drogba. Nahodha huyo wa Ivory na Mourinho walikuwa marafiki walipokuwa Chelsea.
Alisema alipata upinzani mkali kwa Drogba kabla ya kumgeukia Adebayor ambaye alidai Manchester City ilishindwa kuweka bayana kiasi cha fedha inazotaka.
Mourinho alidai alifikiria kuwasajili Karim Benzema na Gonzalo Higuain. "Ukiwa kocha huwezi kuridhika kila mara, tunataka kusajili wachezaji wapya," alisema Mourinho.
Kocha huyo ambaye amepata presha baada ya Real Madrid kulazimishwa suluhu na Mallorca katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu, aliongeza suala la usajili ni gumu.
Mourinho alikiri kukabiliana na changamoto mpya baada ya kutua Real Madrid na kuongeza presha hiyo inatokana na rekodi yake tangu alipokuwa FC Porto, Chelsea na Inter Milan.
No comments:
Post a Comment