Tuesday, August 31, 2010

SIMBA KUKIPIGA NA ULINZI TAIFA.

TIMU ya soka ya Simba inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya timu ya Ulinzi kutoka Kenya, Septemba 4 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa klabu hiyo Ismail Rage alisema mchezo huo utakuwa ni kipimo cha mandalizi ya mashindano ya kimataifa klabu bingwa Afrika itakayochezwa baadae.

Alisema taarifa nyingine kuhusu viingilio pamoja na lini timu ya Ulinzi itawasili itatolewa baadae na vyombo vya habari ambapo timu inatarajiwa pia kujipima ubavu kwa kucheza na timu ya Yanga.

Alisema pia kikosi cha Simba kinatarajiwa kuondoka kuondoka Septemba 5 kuelekea katika kituo chake kipya cha Mwanza ambapo ndipo itakapokuwa ikicheza michezo yake ya nyumbani ikitumia Uwanja wa CCM, Kirumba.

Wakati huohuo Rage alisema klabu hiyo bado inaona vilabu vya Ligi Kuu Tanzania Bara vinaonewa kwa kukatwa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) na Mamlaka ya Mapato (TRA).

Alisema kwa mujibu wa sheria za makato ya kodi inasema kwamba anayepaswa kulipa VAT ni yule ambaye amesajiliwa na TRA na si vinginevyo.

Alisema akifafanua kuwa uongozi wa klabu hiyo umechunguza suala hilo kwa kina na kuona kwamba vilabu vyote vya Ligi Kuu havijasajiliwa na TRA zaidi ya Shikisho la Soka nchini (TFF) wenyewe ambao ndio wamesajiliwa hivyo haoni mantiki ya wao kukatwa kodi.

No comments:

Post a Comment