Monday, August 30, 2010
BARCELONA YAUA, MADRID YANG'AMG'ANIWA
BARCELONA imeanza vyema kutetea ubingwa wake baada ya juzi kuibamiza Racing Santander mabao 3-0 katika mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Santander Sardinero.
Mwanasoka bora wa dunia 2009, Lionel Messi, Andres Iniesta na David Villa, waliifungia Barcelona mabao hayo. Mahasimu wao wakubwa Real Madrid walilazimishwa suluhu na Mallorca.
Matokeo hayo ni mwanzo mbaya kwa Jose Mourinho aliyetua Real Madrid akitokea Inter Milan. "Timu hii tayari nzuri na kila kitu kinawezekana, kwa msingi huo huu ni mwanzo mzuri," alisema Villa.
Villa alifunga bao lake la kwanza Barcelona kwa ligi ya Hispania baada ya kutua Nou Camp katika usajili wa majira ya kiangazi.
Katika mchezo mwingine, Cristiano Ronaldo na Lassana Diara, waliumia katika mchezo dhidi ya Mallorca na kumpa hofu Mourinho.
Ronaldo aliumia kifundo cha mguu wa kulia katika mchezo huo na jana alitarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kina kuhusu maumivu yake. Nahodha huyo wa Ureno, atakosa michezo miwili ya kufuzu fainali za Kombe la Ulaya 2012 dhidi ya Cyprus na Norway.
Diarra ana hofu ya kuitumikia Ufaransa baada ya kuumia uvungu wa goti la kulia. Kiungo huyo alitarajiwa kufanyiwa uchunguzi kabla ya madaktari kutoa tathimini ya maumivu yake
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment