Monday, August 30, 2010
ROBBEN NJE MPAKA MWAKANI.
KLABU ya Bayern Munich huenda ikamkosa mshambuliaji wake nyota, Arjen Robben hadi mwakani baada ya kuumia uvungu wa goti.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Bayern Munich, Christian Nerlinger alisema mkongwe huyo wa Uholanzi amepata maumivu makali na atakuwa nje ya uwanja mude mrfu kabla ya kupona.
Alisema nguli huyo pia anakabiliwa na maumivu ya misuli yaliyoanza kumsumbua muda mfupi kabla ya kuanza fainali za Kombe la Dunia zilizomalizika Julai 11, Afrika Kusini.
Bayern Munich iliwahi kupeleka malalamiko Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), kuishitaki Uholanzi kupinga kumtumia Robben katika fainali hizo ambapo kikosi hicho kilichapwa bao 1-0 na Hispania katika mechi ya fainali. Robben amefunga mabao 16 msimu uliopita.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment