KOCHA wa timu ya Taifa ya Uingereza Fabio Capello alitangaza kikosi cha wachezaji 24 kitakachokuwa kikisaka tiketi kucheza michuano ya Ulaya (Euro 2012).
Wachezaji wawili wa Tottenham Jermain Defoe na Peter Cruoch ni miongoni mwa wachezaji waliorudishwa baada ya kuachwa katika mechi ya kirafiki dhidi ya Hungary.
Shaun Wright-Philips nae ameitwa katika kikosi hicho lakini mshambuliaji aliyetia saini katika klabu ya Liverpool msimu huu Joe Cole ameachwa na Capello.
Kikosi hicho kinakabiliwa na mchezo dhidi ya Bulgaria Septemba 3 mchezo utakaochezwa Uwanja wa Wembley ikifuatiwa na mchezo dhidi ya Switzerland mchezo utakaofanyika Basel Septemba 7.
Mchezo huo ni wa kwanza wa ushindani toka timu hiyo ifanye vibaya katika Kombe la Dunia huko Afrika Kusini.
Kikosi hicho pia kitakuwa bila ya wachezaji wake tegemeo Frank Lampard na John Terry ambao walipatwa na majeruhi wakati wakiitumikia klabu yao ya Chelsea.
Lakini pamoja na kuanza vibaya msimu huu kwa timu ya West Ham, Capello amewaita wachezaji mahiri wa klabu hiyo Matthew Upson na Carlton Cole.
Capello ambaye alishambuliwa wapenzi wa soka wa nchi hiyo kwa kauli yake dhidi ya mchezaji mkongwe wa nchi hiyo David Beckham wakati akihojiwa katika luninga kabla ya mchezo dhidi ya Hungary.
Muitaliano huyo alijirekebisha kwa kusema kuwa hakumaanisha kwamba anamuondoa moja kwa moja kikosini mchezaji huyo.
Capello alisema "Milango iko wazi kwa wachezaji wote lakini hivi sasa nafikiri kuhusu wachezaji wachanga. Wanahitaji kucheza zaidi ili kupata uzoefu. Tunajua umuhimu wa wachezaji wazoefu"
Kikosi cha England kitawakilishwa na:
Makipa: Scott Carson, Ben Foster, Joe Hart
Mabeki: Gary Cahill, Ashley Cole, Michael Dawson, Kieran Gibbs, Phil Jagielka, Glen Johnson, Joleon Lescott, Matthew Upson
Viungo: Gareth Barry, Michael Carrick, Steven Gerrard, Adam Johnson, James Milner, Theo Walcott, Shaun Wright-Phillips, Ashley Young
Washambuliaji: Darren Bent, Carlton Cole, Peter Crouch, Jermain Defoe, Wayne Rooney
No comments:
Post a Comment