Sunday, August 29, 2010

LIVERPOOL YASHINDA, MAN CITY YAPATA KICHAPO.

HATIMAYE Liverpool waliona mwezi baada ya kupata ushindi wa kwanza toka Ligi Kuu ya uingereza ianze kutimua vumbi msimu huu.


Alikuwa ni kiungo Fernando Torres aliyeifungia bao klabu yake hiyo na kufanya Liverpool kutoka kifua mbele kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya West Brom katika Uwanja wa Anfield.

Baada ya kufanyiwa operesheni mara mbili ya magoti msimu uliopita na kuchelewa kurudi kutoka katika fainali za Kombe la Dunia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ameonekana kurudi kurudi katika kiwango chake.

Bao safi aliloshinda katika kipindi cha pili ambalo ni la kwanza kushinda katika timu hiyo toka Machi mwaka huu na la 50 kwa mashindano yote akiwa na klabu hiyo limeonyesha ubora wake.

Wakati Liverpool wakisherekea ushindi wao, Manchester City walipata mshtuko wa mwaka walipokubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya timu ya Sunderland.

Alikuwa ni mshambuliaji Darren Bent aliyepeleka kilio City kwa kufunga bao la penati dakika ya 90 baada ya kuangushwa katika eneo la hatari na Micah Richards na kumaliza uteja wa miaka kumi ya kufungwa na City.

Michezo mingine iliyochezwa leo ni pamoja na Aston Villa 1-0 Everton na Bolton Wanderers 2-2 Birmigham City.

No comments:

Post a Comment