KIUNGO wa timu ya Arsenal and Uingereza Jack Wilshere alikamatwa na polisi kufuatia tukio ambalo mwanamke alivunjwa mkono katika klabu ya usiku huko London.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 18 alikamatwa mapema leo asubuhi lakini aliachiwa baadaye kwa dhamana akituhumiwa kwa kosa kushambulia.
Maofisa na watu wa huduma ya kwanza waliitwa eneo la tukio na kukuta mwanaume akiwa na majeraha ya kawaida pamoja na mwanamke aliyekuwa amevunjika mkono. Wote walipelekwa hospitali huko magharibi mwa London kwa matibabu.
Baadaye poilisi walisimamisha gari na kuwakamata wanaume wanne wawili kati yao wakiwa na umri wa miaka 18 na wengine 21 wakiwahisi kuhusika na shambulio hilo.
"Vijana hao walichukuliwa na kupelekwa kituo cha polisi kilichopo magharibi mwa London na kuachiwa kwa dhamana ambapo walitakiwa kuripoti katikati mwa Octoba kwa ajili ya kuhojiwa zaidi" alisema msemaji wa polisi.
"Mojawapo kati ya vijana waliokamatwa leo asubuhi alikuwapo Wilshere lakini aliachiwa kwa dhamana baadae" alisema msemaji wa mchezaji huyo.
Mchezaji huyo alisema kwamba atatoa ushirikiano wa kutosha kwa polishi ili kumaliza utata wa tukio hilo.
No comments:
Post a Comment