Sunday, August 29, 2010

Sneijder: Mourinho ataifundisha United




Wesley Sneijder anaamini ya kuwa kocha Jose Mourinho atakuwa ndiye mrithi wa  Sir Alex Ferguson katika klabu ya mashetani wekundu Manchester United kama Mscot huyo ataachia ngazi.

Ferguson amekuwa akiifundisha klabu hiyo kwa kipindi cha miaka 24 na kuwa kocha mwenye mafanikio makubwa katika historia ya klabu hiyo.

Bado kumekuwa na tetesi juu ya nani atakuwa mrithi wa Furguson.
Kwa upande wake  Sneijder ambaye katika michuano ya ligi ya mabingwa ulaya msimu uliopita alikuwa katika kikosi cha kocha  Mourinho wakati huo akiwa  Inter Milan anasema self-styled 'Special One' kwasasa anataka kazi Old Trafford.

Mdutch huyo ambaye alingara katika fainali za kombe la dunia akizungumza na  Daily Star hii leo amesema

Nimekuwa n a mazungumzo ya kina na Jose na niko tayari kuweka pesa mezani juu ya Mourinho kuchukua nafasi ya Ferguson(kamari). Najua nafasi anayoitaka kwasasa ni kuwa meneja wa Manchester United.


Kama  Ferguson anastaafu kilichopo akilini mwangu ni kwamba ,mpango mzima umekwisha kamilika na iko hivyo . One world-class manager leaves and another one takes over.

Najua  Alex Ferguson atakuwa na mengi ya kuzungumza juu ya nani wa kuchukua nafasi yake  hata kama wanatofautiana lakini bado kuna heshima kubwa kati yao.'
'
Mourinho akiwa sasa ni charge wa Real Madrid aeshakuwa na matamanio ya kurejea Premier League kufuatia kumbukumbu ya mafanikio akiwa na  Chelsea.

No comments:

Post a Comment