MICHUANO mikubwa duniani ya mchezo wa soka ya UEFA Champions League inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 14 mwaka huu, ambapo droo tayari imeshatangazwa.
Je kikosi cha Inter Milan ambao ni mabingwa watetezi wataweza kutetea ubingwa huo bila Meneja wake Jose Muorinho ambaye ameihama klabu hiyo?
Nao Real Madrid ambao walipata bahati ya kupata saini ya Mourinho au "The special one" pamoja na kikosi chake kilichosheheni nyota wa dunia wataweza kufika fainali ya michuano hiyo?
Pamoja na klabu ya Barcelona kukabiliwa na madeni lakini kikosi chake bado kitaendelea kuwa tishio katika mashindano hayo huku klabu za England Chelsea na Manchester United wakipigana vikumbo na timu zingine za Ulaya kufukuzia nafasi za juu.
Bila kuwasahau washindi wa pili Bayern Munich ambao nao sio wa kubeza haswa ikizingatiwa kwamba walichukua vikombe viwili msimu uliopita huko ujerumani.
Tukiachana na yaliyotokea msimu uliopita, mwaka huu inaonekana kutakuwa na ushindani mkubwa katika mashindano hayo kama makundi yanavyoonekana hapo chini.
Group A
Inter Milan
Werder Bremen
Tottenham
Twente
Group B
Lyon
Benfica
Schalke
H. Tel-Aviv
Group C
Manchester United
Valencia
Rangers
Bursaspor
Group D
Barcelona
Panathinaikos
Kobenahvn
Rubin Kazan
Group E
Bayern Munich
Roma
Basel
CFR Cluj
Group F
Chelsea
Marseille
Spartak Moskva
Zilina
Group G
Milan
Real Madrid
Ajax
Auxerre
Group H
Arsenal
Shakhtar Donetsk
Braga
Partizan
No comments:
Post a Comment