Friday, August 27, 2010
LIVERPOOL YASALIMU AMRI KWA MASCHERANO.
HATIMAYE klabu ya Liverpool imesalimu amri kwa kiungo wake Javier Mascherano baada ya kumruhusu kuanza mazungumzo na klabu ya Barcelona kuhusiana na uhamisho wake.
Kiungo huyo ambaye pia ni nahodha wa Argentina amekuwa akihusishwa na suala la kuondoka katika klabu hiyo kwa muda mrefu toka dirisha la usajili katika majira ya joto lilipofunguliwa ambapo klabu za Barca na Inter Milan zote zilionyesha nia ya kumnyakua.
Mascherano hakuhusishwa katika kikosi cha Liverpool kilichochapwa mabao 3-0 na Manchester City Jumatatu iliyopita baada ya kumfahamisha kocha wake Hudgson kutomjumuisha katika kikosi hicho.
Bosi huyo wa zamani wa klabu ya Fulham aliweka wazi suala hilo baada ya timu hiyo kujihakikishia nafasi ya hatua ya makundi ya ligi ya Ulaya maarufu kama "Europa League" kwamba klabu ilikataa ofa ya Inter Milan ambayo inanolewa na bosi wa zamani wa klabu hiyo Rafa Benitez.
"Liverpool imekubali kumuachia kiungo Javier Mascherano kwenda klabu ya Barcelona na mazungumzo yameshaanza tayari" ilisomeka taarifa kutoka website ya klabu.
Barca watalazimika kulipa kitita cha paundi milioni 16, na kiasi cha paundi milioni 6 kitaongezeka kulingana na kiwango atakachoonyesha mchezaji huo. Anatarajia kusaini mkataba wa miaka minne.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment