Saturday, August 28, 2010

FERGUSON AMKINGIA KIFUA KINDA LAKE JIPYA

KOCHA wa timu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson amekuwa akimkingia kifua kinda lake jipya Bebe alilolisajili kwamba itakuwa ni hazina nzuri kwa klabu hiyo katika kipindi kijacho.


Bebe amekuwa akikingiwa mwavuli toka atue katika klabu hiyo akitokea timu ya Guimaraes ya Ureno kwa ada ya paundi milioni 7.4 katika kipindi cha majira ya kiangazi.

Mchezaji huyo bado hajawa katika mipango ya Ferguson katika kikosi cha kwanza lakini pia ilishangaza kukosekana kwake hata kwenye list ya wachezaji wa akiba katikati ya wiki.

Lakini Ferguson alisema kuwa mchezaji huyo bado hana mazoezi ya kutosha na wameamua kumpa mazoezi maalum kumrudisha katika kiwango kama wachezaji wengine.

"Kwa kifupi ni kwamba Bebe ana uwezo mkubwa na ni mmaliziaji mzuri na hilo limekuwa likinivutia" alisema Ferguson.

No comments:

Post a Comment