BAADA minong'ono ya muda mrefu kuhusu uwezekano kwa Didier Drogba kujitoa katika timu ya Taifa ya Ivory Coast "The Elephant", hatimaye imekuwa kweli. Kocha wa timu hiyo Francois Zahoui aliwaambia waandishi wa habari mjini Abidjan kwamba safari yake ya mjini London kwenda kumshawishi mchezaji huyo iligonga mwamba.
Zahoui alimtembelea mchezaji huyo ili kumambia ajiunge na timu hiyo kwa ajili ya mchezo wa kusaka tiketi ya kucheza Michuano ya Mataifa ya Afrika dhidi ya Rwanda, mshambuliaji huyo anayechezea klabu ya Chelsea alikataa kwa kutoa taarifa za kusikitisha kuhusu kujiondoa kwake kwenye kikosi hicho.
"Ni kweli nilimtembelea Drogba na aliniambia kuwa amechoka na nataka kujiondoa timu ya Taifa kwa muda. Drogba ni mchezaji bora duniani na pengo lake ni ni vigumu kuzibika katika kikosi cha Elephants, lakini nalazimika kuheshimu maamuzi yake. Tutamwacha apumzike ili kurudisha nguvu kimwili na kiakili na tuanaomba atarudi mapema siku zijazo katika kikosi cha Taifa" alisema Zahoui.
Hatahivyo, wachambuzi wa michezo nchini Ivory Coast wanasema mchezaji sio kwamba amechoka kama anavyosema ila ana mawazo juu ya ugomvi usioisha na shirikisho la Soka la Uingereza (FA) na muundo wa timu yake.
Lakini Rais wa FA Jacques Anoma aliondoa wasiwasi huo kwa kusema kuwa ahawana matatizo yoyote na mchezaji huyo.
No comments:
Post a Comment