Monday, August 30, 2010

MASCHERANO ALAMBA MKATABA WA MIAKA MINNE BARCA.


BARCELONA wamethibitisha kuwa tayari wameshafanikiwa kupata saini ya kiungo Javier Mascherano kutoka Liverpool ya miaka minne taarifa ya mtandao wa klabu hiyo ilisema lakini haikuweka wazi kiasi ambacho wamewalipa Liver.


Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Argentina alifaulu vipimo vya afya Jumatatu asubuhi katika klabu hiyo na kukamilisha uhamisho wake kutoka Anfield. Ripoti hiyo ilikisia kwamba Liverpool wamelipwa erou milioni 21.

"Mascherano sasa ni mchezaji rasmi wa Barca baada ya kutia saini mkataba wa miaka minne Jumatatu mchana na klabu hiyo" ilisema taarifa ya mtandao.

Mchezaji huyo ataungana na David Villa na Adriano wakiwa wachezaji wapya waliosaini mikataba na klabu hiyo na kufanya itumie kiasi cha erou milioni 70.5 kwa kununua wachezaji msimu huu.

No comments:

Post a Comment