Mshambuliaji wa Arsenal Robin van Persie atakuwa nje ya uwanja kwa wiki kadhaa kuokana na maumivu ya kifundo cha mguu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 aliumia wakati timu yake iliposhinda mabao 2-1 katika wa Ligi Kuu dhidi ya Blackburn, Jumamosi iliyopita.
Van Persie atakosa mechi ambazo timu yake Taifa ya Uholanzi itacheza kusaka tiketi ya kucheza michuano ya Ulaya dhidi ya San Mario na Finland.
Msimu uliopita mchezaji huyo hakucheza kwa miezi mitano kufuatia majeraha ya kifundo cha mguu tena aliyopata wakati akiitumikia timu yake ya Taifa.
No comments:
Post a Comment