KOCHA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amemtupia ndoano kiungo chipukizi wa Everton, Jack Rodwell (19) akitaka kumsajili majira ya kiangazi kabla ya dirisha la usajili kufungwa rasmi leo.
Ferguson ameahidi kutoa pauni milioni 10 (sh. bilioni 23) pamoja na kiungo wa kimataifa wa England, Michael Carrick. Everton imeonyesha nia ya kutaka kiungo huyo abaki Goodson Park lakini itaangalia ofa ya United.
Rodwell anayecheza timu ya taifa ya England chini ya miaka 21, ana kipaji cha kucheza nafasi ya kiungo mkakaji na beki wa kati, amekuwa na mvuto kwa Ferguson anayetaka kumjenga ili kumrithi beki mkongwe Rio Ferdinand anayekabiliwa na majeruhi muda mrefu.
Ferguson amefananisha kipaji cha kinda huyo na Ferdinand alipokuwa beki chipuziki wa Leeds United kabla ya kumsajili. Nguli huyo anashikilia rekodi ya beki ghali zaidi duniani.
United inataka kumsajili kabla ya dirisha kufungwa ikihofia kulipa fedha nyingi katika usajili wa dirisha dogo. Rodwell aliwahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa Ulaya alipokuwa na miaka 16.
No comments:
Post a Comment