Saturday, August 28, 2010

LAMPARD, TERRY NJE KIKOSI CHA ENGLAND

NYOTA wa Chelsea Frank Lampard and John Terry wameondolewa katika kikosi cha timu ya Taifa ya England kitakachomenyana na Bulgaria na Switzerland katika kusaka tiketi ya kucheza michuano ya Ulaya 2012 kutokana na kuwa majeruhi.


Baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Stoke City, Kocha wa Blues Carlo Ancelotti alisema Lampard anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa ngiri (hernia) wiki ijayo.

Pia taarifa ya klabu hiyo ilifanua kuwa Terry naye atakuwa nje kutokana na matatizo ya kifundo cha mguu wa kulia pamoja na maumivu ya misuli.

Mbali na wachezaji hao pia Bobby Zamora na Peter Crouch nao wako katika hatihati kucheza katika mechi hizo zitakazochezwa Septemba 3 na 7.

Lakini kukosekana kwa Lampard na Terry katika kikosi hicho kunaonekana kumuumiza kichwa kocha Fabio Capello kutokana na mechi zilizopo mbele yake haswa ikizingatiwa kuwa ndio mechi za mwanzo za ushindani toka wachabangwe mabao 4-1 na Ujerumani kwenye Kombe la Dunia hatua ya kumi na sita bora Juni mwaka huu.

"Terry ameshazungumza na uongozi wa timu ya Taifa na madaktari wa Chelsea na timu ya taifa wote wameshajulishwa" ilisema taarifa kutoka tovuti ya klabu.

"Wote wamekubali kuwa Terry ni majeruhi toka mwanzoni mwa msimu na kwamba itakuwa ni vizuri akipata kipindi cha kupumzika kuuguza majeraha yake hayo".

No comments:

Post a Comment