Saturday, August 28, 2010

VIGOGO LIGI KUU ENGLAND VYAENDELEA KUTESA

MABAO ya Theo Walcott na Adrew Arshavin yaliiwezesha Arsenal kuibuka kidedea ugenini dhidi ya timu ngumu ya Blackburn Rovers katika Uwanja wa Ewood Park.


Walcott ndie alifungua pazia la mabao kwa timu hiyo katika dakika ya 19 tokea mchezo huo uanze ambapo kikosi kilifanya kazi kubwa kuhakikisha kinaondoka na pointi zote tatu.

Mchezaji huyo kinda alifunga bao hilo kufuatia pasi nzuri ya Robin van Persie aliyompasia akiwa wingi ya kulia ambapo aliingia nayo ndani na kupiga shuti jepesi lilimpita mlinda mlango wa Rovers Paul Robinson.

Rovers nao hawakukubali kuwaachia vijana wa Arsene Wenger kushinda kirahisi baada ya Mame Diouf kuisawazishia timu yake bao dakika ya 26.

Vijana wa Wenger hawakukata tamaa ambapo Arshavin aliihakikishia timu yake pointi zote tatu baada ya kufunga bao la kuongoza dakika ya 51.

Matokeo mengine ya mechi zilizochezwa jana ni kama ifuatavyo:- Manchester United 3-0 West Ham United, Chelsea 2-0 Stoke City, Blackpool 2-2 Fulham, Wolverhampton Wanderers 1-1 Newcastle, Tottenham hotspurs 0-1 Wigan Athletic.

Mechi za ambazo zitachezwa Jumapili ni pamoja na Bolton vs Birmigham, Liverpool vs WBA, Sunderland vs Manchester City na Aston Villa vs Everton.

No comments:

Post a Comment